Friday, April 25, 2014

Maalim Seif ashambuliwa - Adaiwa kuiba waraka

Maalim Seif ashambuliwa - Adaiwa kuiba waraka
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Utetezi wa muundo wa Muungano wa serikali mbili katika mjadala wa katiba jana ulichukua sura mpya kwa kuelekeza mashambulizi mengi dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ni mtu kigeugeua sawa na kinyonga. Mashambulizi hayo yalianza asubuhi wakati Mohammed Seif Khatib alijadili sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba, akimwelezea Maalim Seif kuwa ni mtu anayebadilika kama kinyonga, kiasi cha kudirikia kuiba nyaraka Ikulu iliku kuulinda Muungano wa serikali mbili, lakini sasa amegeuka na kusaka serikali tatu na Muungano wa mkataba.
Khatib alisema kuwa Maalim Seif aliwachongea viongozi wa Zanzibar, akiwamo Rais wa awamu ya pili, Abood Jumbe, ili kutetea Muungano wa serikali mbili. Mbali na Jumbe, wengine wanaodaiwa kuchongewa na Maalim Seif mwaka 1984, ni Waziri Kiongozi mstaafu, Ramadhani Haji Fakhi, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wolfgang Dourado, wa wakati huo. Alisema Maalim Seif aliwashitaki viongozi hao kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho mwaka huo akidai kwamba walitaka kubadilisha katiba na kuwa na Muungano wa serikali tatu. Khatib alisema Maalim Seif alidai kuwa Dourado alikuwa anasafiri kati ya London na Zanzibar ili kukashifu viongozi wa Muungano na kuwachochea watu wauchukie kuwa siyo wa halali.

0 comments:

Post a Comment