Tuesday, February 17, 2015

HATARIII: KIJANA AINGIZWA MOCHWARI AKIDHANIWA AMEKUFA KUMBE MZIMA...MSIKIE KAULI YAKE HAP




Kijana mmoja, Omary Ramadhani, 28, (pichani) mkazi wa Sinza Madukani, Dar amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya kugongwa na ‘Break Down’ alipokuwa akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi, Mwenge, jijini Dar es Salaam.



Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari hilo hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka apimwe.




Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo, Omary alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa shida.



Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.



Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia tena.



Alisema alipata matibabu kwa muda wa miezi sita ndipo aliruhusiwa kuondoka lakini alitakiwa atoe shilingi 1,000,000 kwa ajili ya tiba maalum kwenye mashine ambayo siijui jina, lakini nimeshindwa kuzipata na ndugu zangu ni walalahoi.

Omary alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki sawasawa na akienda maliwatoni huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo hutoka kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa anapata mara moja kwa wiki.



Omary amewaomba Watanzania wenye moyo wa huruma kumchangia ili atibiwe, aepukane na mateso makali anayopata. Namba yake ni 0656 168 034

0 comments:

Post a Comment